Tazama Mama Mwanao

Tazama Mama Mwanao
ChoirSt. Patrick Morogoro
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Tazama Mama Mwanao Lyrics

Tazama Mama mwanao, atundikwa msalabani
Sababu gani hi-yo, mwanao kutiwa hatiani
{ Uchungu, mama, uchung,u mama,
Uchungu mama kwa mwanao } *2

 1. [ s ] Sioni kosa lolote, alilolitenda mwanangu
  Mwanangu hakuwa na kosa, makosa hayo juu yenu
  Uchungu, uchungu, uchungu sana kwa mwanangu *2
 2. [ t ] Kutundikwa juu msalabani, sababu yake ukombozi
  Atukomboe utumwani, tuwe wana wa ukombozi
  Ni sisi, ni sisi, ni sisi mama wakosefu *2
 3. [ s ] Mwanangu haikumpasa, kufa bure bila sababu
  Mwanangu Mungu mtu pekee, kwake sioni kosa kwangu
  Uchungu, uchungu, uchungu sana kwa mwanangu *2
 4. [ t ] Kumbuka mama Maria, maneno ya mwanao Yesu
  Nitakufa nitafufuka, na kwenda juu kwa Baba yangu
  Ya nini, ya nini, ya nini mama huzuni hiyo