Tumekosa Kweli Tumekosa
| Tumekosa Kweli Tumekosa | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 4,892 | 
Tumekosa Kweli Tumekosa Lyrics
- Tumekosa Kweli tumekosa
 Tunaomba Bwana Tusamehe
 Makosa yetu twayatubu
- Tumekukosea Bwana, tukafuata njia zetu
 Tukakuacha ee Bwana
- Tumekukosea Bwana, tukafuata makosa yetu
 Utusamehe Bwana
- Tumekukosea Bwana, twajifanya wa hekima
 Twakuzidi ee Bwana
- Tumekukosea Bwana, twajifanya ni miungu
 Yetu sisi wenyewe
- Tumekukosea Bwana, twachukua nafasi yako
 Ukawa chini yetu
- Tumekukosea Bwana, twajifanya twalingana
 Na wewe Mungu wetu
- , Tumekukosea Bwana, twajifanya tuna nguvu
 Twakushinda ee Mungu
- Tumekukosea Bwana, tumekosa imani kwako
 Uliye Mungu wetu
- Tumekukosea Bwana, tumekosa tumaini kwako,
 Ewe Muumba wetu
- Tumekukosea Bwana, tumekosa upendo kwako
 Na kwa jirani zetu
 
  
         
                            