Kwa Nini Wanipiga
| Kwa Nini Wanipiga | |
|---|---|
| Performed by | Moyo Mtakatifu wa Yesu Singida | 
| Album | Utukufu wa Bwana | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Composer | G. Mmole | 
| Views | 4,421 | 
Kwa Nini Wanipiga Lyrics
- { Kama nimesema vibaya toa ushahidi wa neno baya
 Bali kama nimesema vema kwanini wanipiga? } *2
- [ s ] Pilato alimhukumu Yesu, ingawa hakuona kosa kwake
 Aliwaogopa Wayahudi, na kubembeleza urafiki wa Kaisari
- Ndugu yangu tafakari kwa makini, mamlaka ulopewa na wenzio
 Unayatumia ipasavyo au waumiza wenzako kama Pilato
- Askari usalama wa raia, acheni kuwadhulumu raia,
 Na kusingizia watu kesi, mnasababisha uvunjaji wa sheria
- Mahakimu na mabingwa wa sheria, haifai kuipotosha sheria,
 Maskini wajane na yatima mnawanyang`anya haki zao hukumuni
- Waganga wakunga na wauguzi, tibuni bila kudai zawadi,
 Watu masikini na yatima wanahangaika vitandani hadi kufa
- Wanandoa tunzeni ahadi zenu, kupendana katika shida na raha,
 Pia kuwalea wana katika njia impasayo Mkristo
- Utoaji wa mimba bila sababu, na kutupa watoto majalalani,
 Ni kutoujali utu wa mtu, na kuwahukumu kifo wasio na kosa
- Dunia yetu inawaka moto, amani yetu imeshatoweka,
 Vita vyatawala kila kona kisa ni tamaa ya mali na madaraka
 
  
         
                            