Misa Centinary

Misa Centinary
Performed by-
CategoryMisa (Sung Mass)
ComposerK'Okeyo
Views20,774

Misa Centinary Lyrics

UTUHURUMIE (MISA CENTINARY)

  1. { Utuhurumie ee Bwana ee
    Ee Bwana (tuhurumie) ee Bwana
    Utuhurumie ee Bwana ee
    eh eh eh - ee Bwana, eh eh eh - ee Bwana } *2
  2. /s/ Ee Kristu tuhurumie, tuhurumie
    Uturumie ee, ee Kristu tuhurumie, ee Kristu tuhurumie
    /a/ Ee Kristu tuhurumie, tuhurumie, ee Kristu tuhurumie,
    Eee Kristu ee Kristu, ee Kristu tuhurumie
    /b/ Ee Kristu, ee Kristu, ee Kristu, ee Kristu,
    Ee Kristu utuhurumie *2
    /t/ Ee Kristu tuhurumie tuhurumie
    Eeh eeh, Ee Kristu tuhurumie
  3. Utuhurumie ee Bwana ee . . .

UTUKUFU KWA MUNGU (MISA CENTINARY)

  1. Utukufu kwa Mungu juu Mbinguni,
    Na amani iwe, kwa watu wenye
    Mapenzi mema duniani kote.

    (Tunakusifu) tunakusifu, tunakuheshimu
    Tunakuabudu, tunakutukuza

  2. Tunakushukuru Mungu kwa ajili,
    Ya utukufu wako, mkuu ee Bwana
    Ni Mungu ndiwe mfalme wa mbinguni.
  3. Ee Baba Mwenyezi Bwana Yesu Kristu,
    Ee mwana wa pekee, ee Mungu Mwana
    Kondoo wa Mungu mwana wake Baba
  4. Mwenye kuondoa dhambi za dunia
    Utuhurumie, tuhurumie
    Maombi yetu Bwana uyapokee
  5. Mwenye kuketi kuume kwa Baba
    Utuhurumie, kwa kuwa ndiwe
    Pekee yako ni mtakatifu
  6. Peke yako Bwana peke yako mkuu
    Ewe Yesu Kristu, pamoja naye
    Roho Mtakatifu milele yote.

NASADIKI KWA MUNGU (MISA CENTINARY)

  1. Nasadiki kwa Mungu mmoja - nasadiki
    Ndiye Baba yetu mwenyezi - nasadiki
    Mwumba mbingu pia dunia - nasadiki
    Nasadiki kwa Yesu Kristu - nasadiki

    Nasadiki (nasadiki) nasadiki nasadiki
  2. Mwana wa pekee wa Mungu -
    Aliyezaliwa kwa Baba -
    Akapata mwili kwa Roho -
    Kazaliwa naye Bikira -
  3. Kisha yeye kasulubiwa -
    Kwa amri ya Ponsio Pilato -
    Kwa ajili yetu kateswa -
    Akafa na akazikwa -
  4. Kafufuka katika wafu -
    Kapaa juu Mbinguni -
    Ameketi kuume kwake -
    Mungu Baba yetu mwenyezi -
  5. Ndipo atakapotokea -
    Kuhukumu wazima na wafu -
    Kwake Roho Mtakatifu -
    Kwa kanisa la Katoliki -
  6. Ushirika wa watakatifu -
    Ondoleo la dhambi zetu -
    Nangojea fufuko wa miili -
    Na uzima wa milele -

MTAKATIFU (MISA CENTINARY)

  • Mtakatifu Mtakatifu,
    Mtakatifu Bwana Mungu
    Mtakatifu Mtakatifu,
    Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi *2
  • Mbingu na dunia zimejaa utukufu
    Mbingu na dunia, mbingu na dunia
    Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako
    Zimejaa utukufu wako

    { Hosanna juu, hosanna juu
    Hosanna juu, hosanna juu mbinguni } *2


    Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina
    Mbarikiwa yeye, mbarikiwa yeye
    Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana
    Ajaye kwa jina la Bwana

FUMBO LA IMANI (MISA CENTINARY)

  • Fumbo la imani
    Fumbo la imani Yesu alikufa
    Fumbo la imani Yesu alifufuka
    Yesu atarudi tena, Yesu atarudi tena

EE MWANAKONDOO (MISA CENTINARY)

  1. Ee Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia ee,
    Ee mwana tuhurumie
    Mwanakondoo wa Mungu ee
    Ee mwana tuhurumie
  2. Ee Mwanakondoo wa Mungu . . .
  3. Mwanakondoo wa Mungu ee,
    Amani utujalie
    Mwenye kuondoa dhambi zetu ee,
    Amani utujalie
    Utujalie amani ee
    A - a -amani, u-utujalie