Misa Fadhili

Misa Fadhili
Performed by-
CategoryMisa (Sung Mass)
Views19,872

Misa Fadhili Lyrics

BWANA UTUHURUMIE (MISA FADHILI)

  1. Bwana Bwana utuhurumie ee Bwana
    Bwana (Bwana) Bwana, Bwana utuhurumie
    (Ee Bwana) - Bwana, Bwana utuhurumie
  2. Kristu Kristu . . .
  3. Bwana Bwana . . .

UTUKUFU (MISA FADHILI)

  1. Utukufu kwa Mungu Mbinguni

    Utukufu (kwako) Mungu Mbinguni
    Na amani (kote) duniani
    Kwa watu wa mapenzi mema.
  2. Tunakuheshimu tunakusifu,
    Tunakuabudu twakutukuza ee Bwana
  3. Tunakushukuru mfalme wa mbingu
    Mwana wa pekee mwana wa Baba ee Bwana
  4. Unayeondoa makosa yetu
    Utuhurumie tusikilize ee Bwana
  5. Kuume kwa Baba unapoketi
    Mtakatifu mkuu tuhurumie ee Bwana
  6. Roho Mtakatifu pamoja nawe,
    Ndani yake Bwana unatukuzwa ee Bwana

NASADIKI KWA MUNGU (MISA FADHILI)

  1. Nasadiki kwa Mungu Baba Mwumba wa vyote
    Nasadiki kwa Yesu Kristu, Mwana wa pekee
    Nasadiki ninasadiki *2
  2. Kwa uwezo wa Roho, Mungu katwaa mwili
    Na hapo Bikira Maria kawa mamaye
  3. Kwa amri ya Ponsyo Pilato, kasulubiwa
    Akafa kazikwa akashukia kuzimu
  4. Siku ya tatu kafufuka kapaa Mbinguni
    Kaketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi
  5. Atarudi siku ya mwisho kutuhukumu
    Nasadiki kwa Roho Mfariji Mtakatifu
  6. Kanisa pia takatifu la Katoliki
    Ushirika wa watakatifu wa Mbinguni
  7. Na maondoleo ya dhambi kwa ubatizo
    Fufuko wa miili uzima wa milele

MTAKATIFU (MISA FADHILI)

  • Mtakatifu, mtakatifu Bwana
    Mtakatifu Mungu wa majeshi
    Mbingu na dunia zimejaa, zimejaa utukufu wako
  • Hosanna *5 Hosanna juu mbinguni *2
  • Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina lake Bwana

FUMBO LA IMANI

  • Ee Bwana tunatangaza kifo chako
    Na kutukuza ufufuko wako
    Mpaka utakapokuja, mpaka utakapokuja

JINA LAKO BABA (MISA FADHILI)

  1. Jina Lako Baba litukuzwe
    Utawale petu milele yote *2
  2. Baba yetu mwema uliye mbinguni
    Jina lako Baba litukuzwe
  3. Na ufalme wako uje hapa kwetu
    Na mapenzi yako yatimilike
  4. Tupe leo mkate wa kila siku
    Tupe leo mkate wa kila siku
  5. Na utusamehe makosa yetu
    Kama tufanyavyo kwa ndugu zetu
  6. Situtie Baba kishawishini
    Bali maovuni utuopoe
  7. Ufalme na nguvu na utukufu
    Vyote vyako Baba hata milele

MWANAKONDOO WA MUNGU (FADHILI)

  1. Mwanakondoo wa Mungu
    Unayeondoa dhambi za dunia ee Bwana
    Tuhurumie, tuhurumie
  2. Mwanakondoo . . .
  3. Mwanakondoo wa Mungu
    Unayeondoa dhambi za dunia ee Bwana
    Tujalie amani