Misa Kariobangi

Misa Kariobangi
Performed by-
CategoryMisa (Sung Mass)
ComposerSamuel Ochieng MakOkeyo
Views21,933

Misa Kariobangi Lyrics

UTUHURUMIE (MISA KARIOBANGI)

  1. [ v ] Utuhurumie
    [ w ] Ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana
    [ v ] Tuhurumie
    [ w ] Ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana, Bwana utuhurumie
  2. Utuhurumie
    Ee Kristu, ee Kristu, ee Kristu
    Tuhurumie
    Ee Kristu, ee Kristu, ee Kristu, Kristu utuhurumie
  3. Utuhurumie - ee Bwana . . .

UTUKUFU JUU (MISA KARIOBANGI)

  1. Utukufu juu kwa Mungu,
    Utukufu juu Mbinguni
    Na amani kote duniani,
    kwa wenye mapenzi mema

  2. Tunakusifu tunakuheshimu,
    Tunakuabudu tunakutukuza
    Twakushukuru kwa ajili,
    Ya utukufu wako mkuu
  3. Ewe Mungu ndiwe mfalme,
    Wa mbinguni Baba Mwenyezi
    Ewe Bwana Yesu Kristu,
    Wa pekee mwana wa baba
  4. Ewe Yesu Mwanakondoo,
    Wa Mungu mwana wa Baba
    Ewe mwenye kuziondoa,
    Dhambi zetu tuhurumie
  5. Ewe mwenye kuziondoa,
    Za dunia dhambi za watu
    Ewe mwenye rehema nyingi,
    Upokee maombi yetu
  6. Uketiye kuume kwake,
    Mungu Baba tuhurumie
    Kwa kuwa ndiwe uliye,
    Peke yako Mtakatifu
  7. Peke yako ni wewe Bwana,
    Peke yako Bwana Mungu
    Peke yako ni Mkombozi,
    Peke yako Yesu Kristu
  8. Naye Roho Mtakatifu,
    Katika utukufu wake
    Mungu mmoja anayeishi,
    Na kutawala milele yote

NASADIKI KWA MUNGU (MISA KARIOBANGI)

  1. Nasadiki kwa Mungu mmoja - ninasadiki
    Ndiye Baba yetu mwenyezi -
    Mwumba mbingu pia dunia -
    Nasadiki kwa Yesu Kristu -

    Nasadiki nasadiki -ninasadiki
    Nasadiki nasadiki -ninasadiki

  2. Mwana wa pekee wa Mungu -
    Mwenye kuzaliwa kwa Baba -
    Akapata mwili kwa Roho -
    Kazaliwa naye Bikira -
  3. Kisha yeye kasulubiwa -
    Kwa amri ya Ponsio Pilato -
    Kwa ajili yetu kateswa -
    Akafa na akazikwa -
  4. Kafufuka katika wafu -
    Kapaa juu Mbinguni -
    Ameketi kuume kwake -
    Mungu Baba yetu Mwenyezi -
  5. Ndipo atakapotokea -
    Kuhukumu wazima na wafu -
    Kwake Roho Mtakatifu -
    Kwa kanisa la Katoliki -
  6. Ushirika wa watakatifu -
    Ondoleo la dhambi zetu -
    Nangojea ufufuko wa miili -
    Na uzima wa milele -

MTAKATIFU (MISA KARIOBANGI)

  • Mtakatifu
    Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu
    Wa majeshi
    Mbingu na dunia zimejaa tukufu wako
  • Hosanna, Hosanna juu Mbinguni
    Hosanna, Hosanna juu Mbinguni
  • Mbarikiwa
    Anayekuja kwa jina lake Bwana Mungu

FUMBO LA IMANI (MISA KARIOBANGI)

  • Kristu - alikufa, Kristu - alifufuka
    Kristu Yesu - alikufa, alifufuka, atakuja tena

BABA YETU (MISA KARIOBANGI)

  1. Baba yetu uliye Mbinguni, Jina lako litukuzwe
    Ufalme wako ufike utakalo lifanyike

  2. Duniani kama Mbinguni -utakalo lifanyike
    Tupe leo mkate wetu -
    Mkate wetu wa kila siku -
  3. Tusamehe makosa yetu -
    Kama vile twawasamehe -
    Waliotukosea sisi -
  4. Situtie majaribuni -
    Walakini utuopoe -
    Maovuni utuopoe -
  5. Kwa kuwa ufalme ni wako -
    Na nguvu na utukufu -
    Utukufu hata milele -

EE MWANAKONDOO (MISA KARIOBANGI)

  1. [ S ] Ee Mwanakondoo
    [ w ] Uondoaye dhambi za dunia utuhurumie } *2
  2. Ee Mwanakondo . . .
  3. Ee Mwanakondoo
    Uondoaye dhambi za dunia utujalie amani
Misa Kariobangi is one of the top widely sung masses in Kenya, known to almost every choir in Kenya.