Misa Taita
Misa Taita Lyrics
BWANA UTUHURUMIE(MISA TAITA)
- Bwana Bwana utuhurumie
Bwana Bwana utuhurumie
Ee Bwana ee, ee Bwana ee!
Ee Bwana utuhurumie
- Kristu Kristu utuhurumie
Kristu Kristu utuhurumie
Ee Kristu ee, ee Kristu ee
Ee Kristu utuhurumie
- Bwana Bwana utuhurumie . . .
TUKUFU (MISA TAITA)
- [ v ] [ w ]
- Tukufu! Tukufu kwa Mungu juu
Amani! Na amani duniani
Kwa watu wenye mapenzi! wenye mapenzi mema *2
A-ma-ni!
- Sifa! Sisi tunakusifu
Heshima! Sisi tunakuheshimu
Tunakuabudu! Sisi tunakuabudu *2
He-shi-ma!
- Tukufu! Sisi tunakutukuza
Shukrani! Sisi tunakushukuru
Kwa ajili ya utukufu! Utukufu wako mkuu *2
Shu-kra-ni!
- EeMungu! Ee Bwana Mungu
Ee Baba! Mfalme wa Mbinguni
Ee Mungu Baba! Mungu Baba Mwenyezi *2
Ee Ba-ba!
- Ee Bwana! Ee Bwana Yesu Kristu
Ee Mwana! Kristu mwana wa pekee
Mwana wa Baba! Mwanakondoo wa Mungu *2
Ee -Mwa-na!
- Mwokozi! Mwenye Kuondoa dhambi
Huruma! Dhambi za dunia
Utuhurumie! Pokea ombi letu *2
Hu-ru-ma!
- Ee Yesu! Kwani ndiwe mtakatifu
Ee Kristu! Kwani ndiwe Bwana
Ewe Yesu Kristu! Ndiwe peke yako mkuu *2
Ee Kri- stu!
- Umoja! Pamoja na Roho Mtakatifu
Milele! Katika utukufu
Tukufu wa Mungu Baba! Kristu anaishi *3
Mi-le-le!
NASADIKI (MISA TAITA)
- Nasadiki kwa Mungu mmoja *2
Mwumba mbingu na dunia *2
Na kwa Bwana Yesu Kristu -
Mwana wake wa pekee
Nasadiki kwa Mungu Baba -
Nasadiki nasadiki Mungu aliyetuumba
Nasadiki nasadiki
Na kwa mwana mkombozi -
Na kwa Roho wa uzima -
- Alitungwa kwa uwezo wake *2
Roho mtakatifu *2
Kazaliwa na Maria
Yule mama na bikira
- Akateswa kwa Pilato ndipo *2
Akasulubiwa *2
Kafa tena akazikwa
Akashuka kuzimu
- Siku ya tatu kafufuka, akapaa *2
Hata mbinguni *2
Amekaa kuume kwa Mungu
Baba aliye Mwenyezi
- Atakuja kuhukumu wazima pia *2
Na wafu *2
Na ufalme utakuwa
falme wake wa milele
- Nasadiki kwa kanisa takatifu *2
Takatifu Katoliki - Katoliki
Shirika la watakatifu
Maondoleo ya dhambi zetu
- Nangojea ufufuko wa miili *2
Toka kwa wafu *2
Na uzima wa milele
Yote hayo nasadiki
MTAKATIFU (MISA TAITA)
- { Mtakatifu Bwana Mungu wetu
Ee, hosanna juu! } *3
Mbinguni - mbinguni
- Utukuzwe Bwana Mungu - ee
Mungu muumba wetu - ee
Mbingu na dunia zimejaa - ee! ee! ee!
Utukufu wako - ee hosanna juu
Ee ee mbinguni - mbinguni
- Utukuzwe Bwana Mungu - ee
Mungu mkombozi wetu - ee
Uliangamiza mauti ukaleta - ee! ee! ee!
Uzima mpya - ee hosanna juu
Ee ee mbinguni - mbinguni
- Utukuzwe Bwana Mungu -ee
Mungu mfariji wetu - ee
Ulimtuma roho kwetu tuwe - ee! ee! ee!
Sote mwili mmoja - ee hosanna juu
Ee ee mbinguni - mbinguni
FUMBO LA IMANI (MISA TAITA)
- Kristu Kristu ee! Kristu alikufa
Kristu Kristu ee! Kristu alifufuka
Kristu, ee Kristu Kristu! Atakuja tena Kristu.
BABA YETU ( MISA TAITA)
Baba yetu uliye mbinguni -
Baba yetu, Baba yetu
- Jina lako litukuzwe daima -
Ee Baba, ee Baba, ee!
Baba yetu uliye mbinguni
Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike
Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni
- Utupe leo mkate wetu wa kila siku
Utusamehe makosa yetu,
Kama tunavyowasamehe
Na sisi waliotukosea,
Usitutie katika kishawishi
Lakini utuopoe maovuni
- Kwani ufalme ni wako - Baba yetu
Kwani nguvu ni zako - Baba yetu
Utukufu ni wako - Baba yetu
Baba milele milele -Hizi zote zako Baba!
MWANAKONDOO (MISA TAITA)
- Mwana - Mwanakondoo wa Mungu
Uondoaye - uondoaye
Dhambi za dunia - dhambi za dunia
Utuhurumie - utuhurumie
- Mwana - Mwanakondoo wa Mungu
Uondoaye - uondoaye
Dhambi za dunia - dhambi za dunia
Utuhurumie - utuhurumie
- Mwana - Mwanakondoo wa Mungu
Uondoaye - uondoaye
Dhambi za dunia - dhambi za dunia
Utujalie - amani