Misa Paulo
Misa Paulo |
---|
Performed by | - |
Category | Misa (Sung Mass) |
Composer | Emmanuel Kilonda |
Views | 3,712 |
Misa Paulo Lyrics
BWANA UTUHURUMIE (MT. PAULO)
- Wewe uliyetumwa kuwaponya wanaojuta dhambi
Ee Bwana utuhurumie, ee Bwana utuhurumie
Bwana, Bwana, ee Bwana, ee Bwana utuhurumie
- Wewe uliyekuja kuwaita wakosefu
Ee Kristu, utuhurumie, ee Kristu, utuhurumie
Kristu, Kristu, ee Kristu, ee Kristu, utuhurumie
- Wewe unayeketi kuume kwa Baba, ukituombea,
Ee Bwana utuhurumie, ee Bwana utuhurumie
Bwana, Bwana, ee Bwana, ee Bwana utuhurumie
UTUKUFU (MISA PAULO)
- Utukufu (utukufu), utukufu (utukufu),
Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
Na amani (na amani) duniani (duniani)
Kwa watu wenye mapenzi mema
- Tunakusifu Bwana, tunakuheshimu,
Tunakuabudu (Bwana), tunakutukuza,
Tunakushukuru (tunakushukuru)
Kwa ajili ya utukufu wako mkuu *4
- Ee Bwana Mungu, Mfalme wa Mbinguni,
Ee ee Bwana Mungu, Mungu Baba Mwenyezi.
Ee Bwana Yesu Kristu, Mwana wa pekee *2
Ee Bwana Mungu, (ee Bwana Mungu)
Mwanakondoo wa Mungu mwana wa Baba *4
- Mwenye kuondoa dhambi za dunia,
Utuhurumie, pokea ombi letu
Ee Mwenye kuketi (ee mwenye kuketi)
Kuume kwa Baba tuhurumie *4
- Kwa kuwa ndiwe, peke yako Mtakatifu,
Peke yako Bwana Mkuu, peke yako Yesu Kristu
Pamoja na roho (Roho Mtakatifu)
Katika utukufu wa Mungu Baba *4
NASADIKI (MT. PAULO)
- Nasadiki - nasadiki, nasadiki - nasadiki *2
- Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi
Muumba wa Mbingu na dunia
Na Yesu Kristu Mwanaye wa pekee,
Mungu kweli na mtu kweli
- Aliyepata mwili kwa uwezo,
Wa Roho Mtakatifu
Kwake yeye Bikira Maria,
Akawa mwanadamu
- Akasulubiwa, akateswa,
Kwa mamlaka ya Ponsyo Pilatu
Na akafa, akazikwa,
Akashuka kuzimuni mmh mmh mmh
- Akafufuka siku ya tatu
Akapaa Mbinguni aah aah
Amekaa kuume kwake Baba
Atakuja tena kuwahukumu, wazima na wafu
- Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,
Kanisa Takatifu Katoliklugha i
Maondoleo ya dhambi, ufufuko wa wafu,
Uzima wa milele Amina
MTAKATIFU (MT. PAULO)
- { Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu
Bwana Mungu wa majeshi } *2
- { Mbingu na dunia zimejaa,
Utukufu wako Bwana } *2
- { Hosanna juu, Hosanna juu
Hosanna juu, Hosanna juu Mbinguni } *2
- { Mbarikiwa anayekuja, kwa jina la Bwana } *2
MWANAKONDOO (MT. PAULO)
- Mwanakondoo, ee Mwanakondoo
Ee Mwanakondoo wa Mungu
Uondoaye dhambi za dunia,
{ Utuhurumie, utuhurumie } *2 huruma!
- Mwanakondoo, ee Mwanakondoo
Ee Mwanakondoo wa Mungu
Uondoaye dhambi za dunia,
{ Utuhurumie, utuhurumie } *2 huruma!
- Mwanakondoo, ee Mwanakondoo
Ee Mwanakondoo wa Mungu
Uondoaye dhambi za dunia,
{ Utujalie amani } *2 amani