Misa ya Mt. Anna

Misa ya Mt. Anna
Performed by-
CategoryMisa (Sung Mass)
ComposerFr. G. F. Kayeta
VideoWatch on YouTube
Views8,204

Misa ya Mt. Anna Lyrics

BWANA UTUHURUMIE (MT. ANNA)

  • { Bwana Bwana, Bwana utuhurumie,
    Bwana utuhurumie utuhurumie
    (Bwana) utuhurumie, tuhurumie Bwana } *2
  • Kristu Kristu utuhurumie *2
    { Ewe Kristu, ewe Kristu, ewe Kristu *2
    Utuhurumie (Kristu) utuhurumie, Kristu tuhurumie } *2
    Kristu utuhurumie, Kristu utuhurumie *2
    Utuhurumie Kristu utuhurumie
  • Bwana utuhurumie . . .

UTUKUFU KWA MUNGU (MT. ANNA)

  • Utukufu, kwa Mungu Mbinguni,
    Na amani dunaini (kwa watu) kwa watu wenye mapenzi mema
  • Tunakusifu tunakuheshimu tunakuabudu tunakutukuza
    Tuankushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu (ee Bwana)
    Ee Bwana Mungu mfalme wa Mbinguni
    (Mungu Baba) Mungu Baba Mwenyezi,
  • Ee Bwana Yesu (Kristu) Mwana wa pekee
    Ee Bwana Mungu Mwanakondoo wa Mungu
    Mwana wa Baba (Mungu) wa Mungu Mwana wa Baba
  • Mwenye kuondoa dhambi za dunia utuhurumie
    Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia
    (pokea) pokea ombi letu
    (ewe) Mwenye kuketi kuume kwa Baba
    Utuhurumie (Bwana) utuhurumie
  • Kwa kuwa ndiwe uliye (peke) peke yako mtakatifu
    (Peke) peke yako Bwana (peke) peke yako mkuu
    (Yesu) Yesu Kristu,
  • Pamoja na Roho Mtakatifu katika utukufu wa Mungu Baba
    Katika utukufu, katika utukufu wa Mungu Baba
    Katika utukufu wa Mungu Baba
    (katika) Utukufu wa Mungu amina amina
    Katika utukufu wa Mungu (Baba) Amina amina

MTAKATIFU (MT. ANNA)

  • {Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu
    Bwana Mungu wa majeshi
    Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi *2 } *2
  • Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako
    Zimejaa utukufu wako
  • { Hosana juu, hosanna juu, hosanna juu,
    hosanna hosanna juu mbinguni *2
  • Mbarikiwa yeye ajaye, ajaye kwa jina la Bwana
    Kwa jina la Bwana
    Yeye ajaye kwa jina la Bwana anayekuja kwa jina la Bwana

MWANAKONDOO (MT. ANNA)

  • { Mwanakondoo wa Mungu,
    uondoaye dhambi za dunia utuhurumie } *2
    Mwanakondoo wa Mungu uondoaye
    { Mwanakondoo wa Mungu,
    uondoaye dhambi za dunia utuhurumie } *2
  • Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia
    Mwanakondoo wa Mungu unayeondoa dhambi
    Utujalie utujhalie utujalie utujalie
    Utujalie Bwana utujalie amani