Misa Rapogi
Misa Rapogi |
---|
Performed by | - |
Category | Misa (Sung Mass) |
Composer | Ochieng Odongo |
Views | 13,836 |
Misa Rapogi Lyrics
BWANA UTUHURUMIE
- Bwana utuhurumie Bwana Ee Bwana
Bwana ee ee ee Bwana utuhurumie *2
- Kristu, utuhurumie ee Kristu
Ee ee Kristu utuhurumie.*2
- Bwana . . .
UTUKUFU KWA MUNGU (RAPOGI)
- Utukufu kwa Mungu juu Mbinguni
Na amani iwe kote duniani,
Kwa watu wenye mapenzi mema
{ Tunakusifu, tunakuheshimu
Na tunakuabudu Baba tunakutukuza } *2
- Tunakushukuru Mungu kwa ajili
Ya utukufu wako mkuu ee Bwana,
Ni Mungu ndiwe mfalme wa Mbingu
- Ee Baba Mwenyezi Bwana Yesu Kristu
Ee Mwana wa pekee ee Mungu Mwana
Kondoo wa Mungu mwana wake Baba.
- Mwenye kuziondoa dhambi za dunia
Utuhurumie tuhurumie
Upokee Baba maombi yetu
- Ewe mwenye kuketi kuume kwa Baba
Utuhurumie kwa kuwa ndiwe
Pekee yako ndiwe mtakatifu
- Pekee yako ndiwe mkuu
Ee Yesu Kristu pamoja naye
Roho Mtakatifu milele yote
BABA YETU (MISA RAPOGI)
Ee Baba, ee Baba yetu,
Baba yetu uliye mbinguni
Jina lako litukuzwe Baba ee baba yetu
Jina lako litukuzwe
- Ufalme wako ufike, utakalo Baba lifanyiike kote
Baba ee baba yetu jina lako litukuzwe
Duniani kama Mbinguni, tupe leo mkate wetu wa kila siku
Baba ee baba yetu jina lako litukuzwe
- Tusamehe makosa yetu, vile twasamehe waliotukosea
Situtie majaribuni, walakini maovuni utuopoe
- Kwa kuwa ufalme ni wako, nguvu utukufu, utukufu milele