Login | Register

Sauti za Kuimba

Misa Rapogi Lyrics

MISA RAPOGI

@ Ochieng Odongo

BWANA UTUHURUMIE

 1. Bwana utuhurumie Bwana Ee Bwana
  Bwana ee ee ee Bwana utuhurumie *2
 2. Kristu, utuhurumie ee Kristu
  Ee ee Kristu utuhurumie.*2
 3. Bwana . . .

  UTUKUFU KWA MUNGU (RAPOGI)

  1. Utukufu kwa Mungu juu Mbinguni
   Na amani iwe kote duniani,
   Kwa watu wenye mapenzi mema

   { Tunakusifu, tunakuheshimu
   Na tunakuabudu Baba tunakutukuza } *2

  2. Tunakushukuru Mungu kwa ajili
   Ya utukufu wako mkuu ee Bwana,
   Ni Mungu ndiwe mfalme wa Mbingu
  3. Ee Baba Mwenyezi Bwana Yesu Kristu
   Ee Mwana wa pekee ee Mungu Mwana
   Kondoo wa Mungu mwana wake Baba.
  4. Mwenye kuziondoa dhambi za dunia
   Utuhurumie tuhurumie
   Upokee Baba maombi yetu
  5. Ewe mwenye kuketi kuume kwa Baba
   Utuhurumie kwa kuwa ndiwe
   Pekee yako ndiwe mtakatifu
  6. Pekee yako ndiwe mkuu
   Ee Yesu Kristu pamoja naye
   Roho Mtakatifu milele yote

   BABA YETU (MISA RAPOGI)

   Ee Baba, ee Baba yetu,
   Baba yetu uliye mbinguni
   Jina lako litukuzwe Baba ee baba yetu
   Jina lako litukuzwe

   1. Ufalme wako ufike, utakalo Baba lifanyiike kote
    Baba ee baba yetu jina lako litukuzwe
    Duniani kama Mbinguni, tupe leo mkate wetu wa kila siku
    Baba ee baba yetu jina lako litukuzwe
   2. Tusamehe makosa yetu, vile twasamehe waliotukosea
    Situtie majaribuni, walakini maovuni utuopoe
   3. Kwa kuwa ufalme ni wako, nguvu utukufu, utukufu milele
   Misa Rapogi
   COMPOSEROchieng Odongo
   CATEGORYMisa (Sung Mass)
   • Comments