Misa Migori
Misa Migori Lyrics
BWANA TUHURUMIE
- Bwana tuhurumie, tuhurumie ewe Bwana Aah aah ah Bwana
Tuhurumie ewe Bwana
- Yesu Kristu tuhurumie . . .
- Bwana tuhurumie
UTUKUFU KWA MUNGU (MIGORI)
Utukufu kwa Mungu juu na amani duniani
Na amani kwa watu wote (wenye)
{ Wenye mapenzi mema, watu wenye mapenzi mema
Wenye mapenzi Watu (wenye) mapenzi mema }*2
- Tunakusifu tunakuheshimu
Tunakuabudu tunakutukuza
Tunakushukuru kwa ajili ya
Utukufu wako, wako mkuu
- Ee Bwana Mungu mfalme wa mbinguni,
Mungu Baba mwenyezi ee Bwana Yesu Kristu,
Mwana wa pekee, ee mwana Mungu
Mwanakondoo wa Mungu, mwana wa Baba
- Mwenye kuondoa dhambi za dunia
Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia
Pokea ombi letu ewe mwenye kuketi
Kuume kwa Baba, utuhurumie
- Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako
Peke yako mkuu ee Bwana Yesu Kristu
Pamoja na Roho Mtakatifu
Katika utukufu, wa Mungu Baba amina