Misa Subukia
Misa Subukia Lyrics
BWANA BWANA UTUHURUMIE
- Bwana, Bwana, Bwana utuhurumie *2
- Kristu utuhurumie, Kristu utuhurumie *2
- Bwana, Bwana, Bwana utuhurumie *2
UTUKUFU JUU KWA MUNGU (SUBUKIA)
{ Utukufu juu kwa Mungu, na amani duniani,
kwao watu wenye mapenzi,
watu wenye mapenzi mema } *2
- Tunakusifu tunakuheshimu, twakuabudu tunakutukuza
Twakushukuru kwa ajili yako, ya utukufu wako mkuu.
- Ee Mungu baba ndiwe mfalme,
Mfalme wa Mbinguni baba mwenyezi.
Ee Yesu Kristu mwana wa pekee,
mwanakondoo mwana wa Baba.
- Uondoaye dhambi za watu tuhurumie tusikilize,
Tuhurumie mwenye rehema maombi yetu uyapokee.
- Uketiye kuume kwake, Mungu baba tuhurumie.
Kwa kuwa ndiwe pekee yako, Pekee yako Mtakatifu.
- Pamoja naye roho Mtakatifu, katika utukufu wake
Anayeishi na kutawala, milele yote Amina.
MTAKATIFU (SUBUKIA)
- Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Mungu wa majeshi
Mbingu na dunia zimejaa, zimejaa utukufu wako.
- Hosanna hosanna hosanna hosanna juu mbinguni
- Mbarikiwa anayekuja anayekuja kwa Jina la Bwana