Niko Tayari Kuhubiri Injili

Niko Tayari Kuhubiri Injili
Performed by-
CategoryInjili na Miito (Gospel)
Views4,592

Niko Tayari Kuhubiri Injili Lyrics

  1. Niko tayari kuhubiri injili, niko tayari niko tayari
    Mahali popote na wakati wowote, niko tayari niko tayari
    Niko tayari kuitangaza neon, neno la Mungu kwa mataifa,
    Mungu Mwenyezi niwekee mikono, nikahubiri nikahubiri

  2. Ninakutegemea Mungu Mwenyezi, ukanilinde uniongoze
    Utume na Roho Mtakatifu, akanijaze niwe imara
    Nikahubiri bila kuwa na woga, wakasikie dunia yote
  3. Niwaamshe wote walio walala, niwaelekeze kwa Mungu wetu
    Niwape nguvu na waliolegea, na wazipate wawe imara
    Na wale wote wakisikia neon, walisikie na watambue
  4. Ninawaomba waumini wenzangu, mkanipe ushirikiano
    Na mema yote nitakayofundisha, mkayashike na kuyaishi
    Na waalika wote tukahubiri, tukahubiri neno la Mungu