Enyi Wakristu Wapenzi

Enyi Wakristu Wapenzi
Performed by-
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerJ. Urassa
Views10,337

Enyi Wakristu Wapenzi Lyrics

  1. { Enyi wakristu wapenzi njooni
    Bwana anatualika kwenye karamu } *2
    Kwanza ndugu tazama meza yake inavyopendeza
    Yeye Bwana na wateule wameizunguka meza yake
    Haya ndugu simama nawe ushiriki *2

  2. Njoni Bwana atuita meza yake sasa itayari
    Haya simama nenda nawe ushiriki
  3. Kama wewe wastahili fanya hima ukampokee
    Ndicho chakula chenye uzima milele
  4. Yeye anilaye mimi atakuwa na uzima mpya
    Siku ya mwisho mimi nitamfufua
  5. Yeye katuandalia masikini pia matajiri
    Ukarimu gani Bwana Yesu alionao