Mimi Ndimi Baba Yao
Mimi Ndimi Baba Yao |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Composer | Martin M. Munywoki |
Views | 2,207 |
Mimi Ndimi Baba Yao Lyrics
{Mimi ndimi Baba yao Baba milele (milele),
nao ni wanangu Nitawasikiliza nitasikia (mimi),
wakinililia katika taabu} *2
- Mimi ndimi wokovu wa watu, nitawaokoa
Wakinililia katika taabu yoyote, nitawasikia
Mimi ndimi aishikaye kweli, nitawahukumu
Walioonewa na taifa lisilo haki, nitawafungua
- Mimi ndimi mchungaji mwe-ema, nitawakusanya
Waliotawanyikia nchi za ugenini, nitawarejesha
Mimi ndimi mwa-limu wa watu, nitawafundisha
Waliolemewa na mizigo yao mizito, nitawapumzisha
- Mimi ndimi m-kate wa uzima, nitawashibisha
Wote wenye njaa na kiu ya haki hakika, nitawashibisha
Mimi ndimi ufufuo wa kweli, nitawafufua
Wakinirudia na kutubu maasi yao, nitawasamehe
- Mimi ndimi kimbilio la watu, nitawahifadhi
Waliotengwa kando na jamaa zao, nitawapokea
Mi-mi ndimi wo-kovu wa watu, nitawaokoa
Wakinililia katika taabu yoyote, nitawasikia