Mshukuruni Bwana

Mshukuruni Bwana
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerP. F. Mwarabu
ReferencePs. 136

Mshukuruni Bwana Lyrics

{ Mshukuruni Bwana, Mshukuruni Bwana Mungu
kwa kuwa ni mwema
Kwa maana fadhili zake ni za milele } *2

 1. Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya Bwana,
  Kuzihubiri sifa zake zote
 2. Akaikemea bahari ya shamu ikakauka
  Akawaongoza vilindini kana kwamba ni mchanga
 3. Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia
  Na kuwakomboa na mkono wa adui zao
 4. Maji yakawafunika watesi wao
  Hakusalia hata mmoja wao