Niseme Nini ee Bwana
   
    
     
         
          
            Niseme Nini ee Bwana Lyrics
 
             
            
- Niseme nini ee Bwana, nitamke maneno gani kinywani
 Nikushukuru jinsi gani,
 Nisimulie vipi mimi, mapito niliyopita kuja hapa
 Nikutukuze vipi Mungu
 Niseme tu, Bwana Mungu wangu, asante nakushukuru
 Narudia, Bwana Mungu wangu, asante nakushukuru
- Nakumbuka nilivyojaribu, sikujua kama utajibu
 Nikapapasa mkono kizani, kulipokucha ni tunda mkononi
- Katikati ya safari maji yale yakamwagika chini
 Lakini kwa wema wako, umeyazoa yakajaa upya
- Nilipigwa mawe nikaaibishwa sana
 Tazama leo umeniona, ukamtukuza mtumishi wako