Login | Register

Sauti za Kuimba

Niseme Nini ee Bwana Lyrics

NISEME NINI EE BWANA

@ Bernard Mukasa

Niseme nini ee Bwana, nitamke maneno gani kinywani
Nikushukuru jinsi gani,
Nisimulie vipi mimi, mapito niliyopita kuja hapa
Nikutukuze vipi Mungu
Niseme tu, Bwana Mungu wangu, asante nakushukuru
Narudia, Bwana Mungu wangu, asante nakushukuru

  1. Nakumbuka nilivyojaribu, sikujua kama utajibu
    Nikapapasa mkono kizani, kulipokucha ni tunda mkononi
  2. Katikati ya safari maji yale yakamwagika chini
    Lakini kwa wema wako, umeyazoa yakajaa upya
  3. Nilipigwa mawe nikaaibishwa sana
    Tazama leo umeniona, ukamtukuza mtumishi wako
Niseme Nini ee Bwana
COMPOSERBernard Mukasa
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE2
4
NOTES Open PDF
  • Comments