Nitakushukuru kwa Moyo Wangu Wote
| Nitakushukuru kwa Moyo Wangu Wote | |
|---|---|
| Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha | 
| Album | Haya Tazameni (Vol 21) | 
| Category | Thanksgiving / Shukrani | 
| Composer | Elias Majaliwa | 
| Views | 9,567 | 
Nitakushukuru kwa Moyo Wangu Wote Lyrics
- { Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote } *2
 { Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi
 Nitashukuru nikilikabili hekalu lako
 Hekalu lako hekalu lako takatifu
 Nitalishukuru jina lako Bwana (Bwana) *2 } *2
- Kwa ajili ya fadhili na uaminifu wako
 Wewe Bwana umeikuza ahadi yako
 Kuliko jina lako na nilipokuita
 Uliitika ukanifariji nafsi
- Ee Bwana wafalme wote watakushukuru
 Watakaposikia maneno ya kinywa chako
 Naam wataziimba njia zako Bwana
 Kwa maana utukufu wako ni mkuu
 
  
         
                            