Nitakusifu Mungu
Nitakusifu Mungu Lyrics
{ Nitakusifu Mungu(Mungu) Mwenyezi
Kwa mema mengi Baba unayoyatenda } *4
{ Unastahili sifa milele (Bwana)
Utukufu na sifa zako milele } *2
- Furaha yangu ni kubwa ee Mungu kukusifu kwa nyimbo nzuri na sala
Unipe neema zako ee Mungu niongoze katika maisha yangu
- Mbingu zahubiri utukufu Mungu wangu bila uoga wowote
Anga yaitangaza kazi ya mikono yako ee Mwenyezi uliye juu
- Fadhili zako ni za milele na uaminifu wako haupimiki
Nitaimba zaburi yako Bwana siku zote za maisha yangu