Mungu Mmoja
| Mungu Mmoja | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Utatu Mtakatifu (Holy Trinity) | 
| Composer | Martin M. Munywoki | 
| Views | 7,371 | 
Mungu Mmoja Lyrics
- Mungu mmoja katika nafsi tatu mamoja, ni fumbo kubwa *2
 { (Kuwa Mungu) Mungu Baba (Mungu) Mungu mwana
 (Mungu) Roho Mtakatifu, Mungu mmoja } *2
- Usifiwe Utatu Mtakatifu, Mungu Baba Mungu Mwana
 Na Roho Mtakatifu, milele na milele
- Usifiwe Mungu Baba yetu, Mungu Muumba mpaji
 Umeziumba mbingu, nchi na vitu vyote
- Usifiwe Mungu Mwana Mwokozi, Mungu kweli mtu kweli
 Uliyetukomboa, kutoka utumwani
- Usifiwe Roho Mtakatifu, mwalimu kiongozi
 Mgavi wa vipaji, pia mfariji wetu
 
  
         
                            