Nampenda Mungu Muumba Wangu
| Nampenda Mungu Muumba Wangu |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Zaburi |
| Composer | A. J. Msangule |
| Views | 6,055 |
Nampenda Mungu Muumba Wangu Lyrics
Nampenda Mungu Muumba wangu, kwa maana amenisikiliza
Amekisikia kilio changu, maombi yangu ameyapokea
{ Nilipokuwa tabuni, Yeye alinishika mkono (tena)
Kifo kiliponisonga, Mungu aliniponya salama } *2
- Hatari ya kifo ilinizunguka na vitisho vya mauti
Vilinivamia nikajawa na mahangaiko ya majonzi
- Nikamlilia Mwenyezi Mungu kwa kelele zenye hofu
Kwa huruma yake akaniponya ee Mungu tegemeo langu
- Mungu huwalinda wanyofu wa moyo wasipatwe na mikasa
Wakikandamizwa huwaokoa maana yeye mwaminifu