Dunia Mti Mkavu
| Dunia Mti Mkavu |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Tafakari |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 4,250 |
Dunia Mti Mkavu Lyrics
- Dunia ni mti mkavu, nimeona nimeamini
Wanaosema ni wajanja sasa nao wapagawa
Ukiuliza mashariki - sijui
Ukiuliza magharibi - sijui
Kaskazini na kusini - sijui
Hata nao pia wanasemezana - sijui
Dunia imebadilika - sijui
Na sisi tutakwenda wapi - sijui
Hiki kiza chatikisa dunia yetu
Twaomba Baba tuonee huruma utuokoe *2
- Mambo mengi yabadilika huku kule kwashangaza
Jibu limekuwa 'sijui' amani yatatanisha
- Tumuombe Mwenyezi Mungu ashushe baraka zake
Ili tuishi kwa amani, dini zote zipendane
- Twaiombea nchi yetu, Baba Mungu uilinde
Uiepushe na majanga na maradhi ya kutisha