Dunia Mti Mkavu Lyrics

DUNIA MTI MKAVU

@ J. C. Shomaly

 1. Dunia ni mti mkavu, nimeona nimeamini
  Wanaosema ni wajanja sasa nao wapagawa

  Ukiuliza mashariki - sijui
  Ukiuliza magharibi - sijui
  Kaskazini na kusini - sijui
  Hata nao pia wanasemezana - sijui
  Dunia imebadilika - sijui
  Na sisi tutakwenda wapi - sijui

  Hiki kiza chatikisa dunia yetu
  Twaomba Baba tuonee huruma utuokoe *2

 2. Mambo mengi yabadilika huku kule kwashangaza
  Jibu limekuwa 'sijui' amani yatatanisha
 3. Tumuombe Mwenyezi Mungu ashushe baraka zake
  Ili tuishi kwa amani, dini zote zipendane
 4. Twaiombea nchi yetu, Baba Mungu uilinde
  Uiepushe na majanga na maradhi ya kutisha
Dunia Mti Mkavu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CATEGORYTafakari
SOURCESt. Paul's Students Choir, University of Nairobi
 • Comments