Palikuwa na Kijana Mmoja
Palikuwa na Kijana Mmoja |
---|
Performed by | - |
Category | Watakatifu |
Composer | (traditional) |
Views | 7,008 |
Palikuwa na Kijana Mmoja Lyrics
- Palikuwa na kijana mmoja jina lake Samweli,
Alikuwa akimcha Mungu tangu utoto wake
Alisikia sauti Ikimwita, Samweli, Samweli *2
- Alikuwa 'kiitwa na Mungu, lakini hakujua,
Alikimbilia kwake Eli, Eli hakuelewa
- Aliitwa naye Mungu tena, wala hakufahamu,
Eli 'kashangaa akasema: Mimi sikukuita
- Alipoitwa mara ya tatu, Samweli akajibu:
Nena, Bwana, mtumishi wako anatega sikio.
- Mungu akawa pamoja naye, na Israeli nzima
Ikafahamu kuwa Samweli ndiye nabii wake