Siku Ile Inayokuja
| Siku Ile Inayokuja |
|---|
| Alt Title | Kwa Maana Angalieni |
| Performed by | - |
| Category | Tafakari |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 2,889 |
Siku Ile Inayokuja Lyrics
Kwa maana angalieni, siku ile inayokuja
Inawaka kama tanuru kama tanuru
Watu wote wenye kiburi, nao watendao uovu
Watakuwa kama makapi, kama makapi
{ Wengi nao watajiuliza, hatukutoa pepo,
Na kwa ji-na la-ko kufa-nya mi-ujiza } *2
- Jiandae ndugu yangu siku hiyo yaja
Kila mtu atalichukua furushi lake
- Jiulize kwa makini utakuwa wapi
Ukiitwa leo au kesho ujiulize
- Siku ile inakuja hatujui saa
Kila mtu atalichukua furushi lake