Tusali Pamoja
Tusali Pamoja |
---|
Alt Title | He Subiri Niwakumbusheni |
Performed by | St. Yuda Thadei Mbeya |
Album | Mlipuko wa Sifa |
Category | Tafakari |
Composer | Gasper Idawa |
Views | 4,602 |
Tusali Pamoja Lyrics
Hee! subiri niwakumbusheni jambo lilo jema wakristu
Kweli tusikie vyema kwa makini
Kweli we kijana wewe Baba mama mtuelewe
Hebu sikia na kutekeleza, hebu sikia na kufanyia kazi
Kanisa litajengwa kwa familia
zinazosali pamoja kwa upendo na
Kukaa kifamilia kushirikishana matatizo yao na kuyatatua
- Jumuiya zetu na ibada mbali mbali
Zimekuwa haswa ni za kina mama
Jumuiya nyingi zimejaa mama zetu
Familia gani zilizokosa baba
- Jumuiya zetu hazina vijana
Familia gani zisizo na vijana
Tumewaachia hasa mama zetu
Kusali si kwa mama ni familia nzima
- Familia yaundwa baba mama na mtoto
Iweje kusali baba haonekani
Kama ni motto yule wa mgongoni
Usiyemuacha peke yake nyumbani
- Vijana ni wengi wapo mitaani
Ukiwafuatafuata wasema wako bize
Wamemsahau hata Mungu wao
Siku wanayojua, Jumapili pekee