Ujana ni Maji Moto Lyrics

UJANA NI MAJI MOTO

@ J. C. Shomaly

Ujana ni maji ya moto bila Mungu ni majuto
Ujana ni maji ya moto ukicheza utakuchoma
Kunapokucha ni raga
Mwili bado una nguvu nyingi
Tunapomsahau Mungu vijana twapotea *2

 1. Vishawishi ni vingi mno, ili tupate pesa nyingi
  Wengine tunaua ili tupate pesa
  Twaharibu amani ili tupate pesa
  Tunapomsahau Mungu vijana twapotea
 2. Magaidi wanatutumia, twauana sisi kwa sisi
  Jamii inalia machozi ya uchungu
  Wasio na hatia wauawa kwa nini
  Tunapomsahau Mungu vijana twapotea
 3. Ndoto zetu zinakatizwa, na wale wasio na utu
  Wasiwasi kazini, wasiwasi shuleni
  Mjini wasiwasi twatembea kwa hofu
  Tunapomsahau Mungu vijana twapotea
Ujana ni Maji Moto
COMPOSERJ. C. Shomaly
CATEGORYTafakari
SOURCESt. Paul's Students Choir, University of Nairobi
 • Comments