Mwasumbukia Mambo Gani
Mwasumbukia Mambo Gani |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Views | 2,831 |
Mwasumbukia Mambo Gani Lyrics
- Enyi wanadamu mwasumbukia mambo gani
Ya Mungu ya Mungu, ya shetani ni ya shetani
Msijisumbue mle nini mvae nini
Kwani Baba yenu wa Mbinguni amewapangia
Tazameni hawa ndege wa angani,
Hawalimi hawavuni, wanaishi,
Ninyi si zaidi ya ndege hawa
Mna haki ya kubarikiwa na Baba yangu *2
- Mnahangaika kufanya kazi kila siku
Na mnazeeka hata bila ya kufanikiwa
Muiteni Mungu kazini hata manyumbani
Atawabariki maisha yenu yawe salama
- Kutwa hata kucha maisha yanawasumbua
Na vijana wenu wamegeuka hohe hahe
Heshima hakuna mmebaki mkiwalilia
Mkabidhi Mungu matatizo ya familia
- Maisha mazuri mnakula mkibakisha
Lakini kwa ndani mawazo yanawamaliza
Usoni ni raha lakini ndani mwaumia
Mkabidhi Mungu matatizo ya kibinafsi
- Mchana wa jua hata usiku wa mbalamwezi
Siyo tofauti kwake yeye asiye na raha
Kukikucha kesho asema afadhali ni jana
Hata kesho kutwa aseme afadhali ni leo
- Yote hayo tisa, la kumi Mungu ndiye dawa
Maisha ya raha bila Mungu yote balaa
Tutubu tuombe raha ije ndani na nje
Tutabarikiwa pia tutamaliza vizuri