Nayaweza Yote
Nayaweza Yote | |
---|---|
Performed by | BMT Ledochowska K/Ndege Dodoma |
Album | Mungu |
Category | Tafakari |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 4,508 |
Nayaweza Yote Lyrics
Nalifurahi sana katika Bwana,
Kwa kuwa mmehuisha fikira zenu
Najua kudhiliwa na kufanikiwa
Kwa hali yoyote na kwa mambo yoyote
Nimefunzwa kushiba na kuona njaa,
Kuwa na vingi na hata kupungukiwa.
(Najua) najua kushiba, (najua) na kuona njaa
(Najua) kuwa navyo vingi, (najua) na kupungukiwa
(Ni)najua (ni) najua mi
Nayaweza - Nayaweza mambo yote
Nayamudu - Nayaweza mambo yote
Ni katika yeye - Nayaweza mambo yote
Anipaye nguvu - Nayaweza mambo yote
Nayaweza - Nayaweza mambo yote- Najua wazi mimi kiumbe dhaifu,
Ni kwake Bwana maisha yangu nayaweka
Sina nguvu nje ya mwokozi,
Ni kwake Bwana maisha yangu nayaweka - Ninaendelea mbele na utumishi -
Kwani Bwana anitia nguvu - - Nimevipiga vita vilivyo vizuri -
Na (mwendo) nimemaliza -
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristu,
Upendo upendo wa Mungu Baba
Na ushirika wa Roho Mtakatifu (viwe nanyi)
Viwe nanyi viwe (sasa) sasa (viwe nanyi)
Sasa hata milele *2