Kabila Langu
| Kabila Langu | |
|---|---|
| Performed by | St. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Composer | Fr. G. F. Kayeta | 
| Views | 5,892 | 
Kabila Langu Lyrics
- { Kabila langu nimekutenda nini
 Au nimekusikitisha nini, nijibu, nijibu } *2
- Kwa kuwa nimekutoa katika nchi ya Misri
 Umemtayarishia mkombozi wako msalaba
- Kwa kuwa nimekuongoza jangwani kwa miaka arobaini
 Umemtayarishia mkombozi wako msalaba
- Ilinipasa kukutendea nini zaidi nisikutendee
 Kweli nimekupenda kama shamba langu nzuri sana
- Mimi nimewapiga Wamisri kwa ajili yako,
 Nawe ukanitoa nipigwe mijeredi.
- Mimi nimekutoa Misri, nikamtoa Farao katika bahari ya Sham,
 Nawe ukanitoa kwa makuhani wakuu.
 
  
         
                            