Kabila Langu Lyrics

KABILA LANGU

@ Fr. G. F. Kayeta

{ Kabila langu nimekutenda nini
Au nimekusikitisha nini, nijibu, nijibu } *2

 1. Kwa kuwa nimekutoa katika nchi ya Misri
  Umemtayarishia mkombozi wako msalaba
 2. Kwa kuwa nimekuongoza jangwani kwa miaka arobaini
  Umemtayarishia mkombozi wako msalaba
 3. Ilinipasa kukutendea nini zaidi nisikutendee
  Kweli nimekupenda kama shamba langu nzuri sana
 4. Mimi nimewapiga Wamisri kwa ajili yako,
  Nawe ukanitoa nipigwe mijeredi.
 5. Mimi nimekutoa Misri, nikamtoa Farao katika bahari ya Sham,
  Nawe ukanitoa kwa makuhani wakuu.
Kabila Langu
COMPOSERFr. G. F. Kayeta
CHOIRSt. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE4
4
NOTES Open PDF
 • Comments