Mtazame Mkombozi Msalabani
| Mtazame Mkombozi Msalabani | |
|---|---|
| Performed by | - |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | (traditional) |
| Views | 2,843 |
Mtazame Mkombozi Msalabani Lyrics
Mtazame Mkombozi msalabani,
Tazama mikono na miguu, vimefungwa kwa misumari
Mtazame Mkombozi msalabani,
Tazama ubavu wake, ulivyochomwa kwa mkuki- Msilie enyi kila mama, msinililieni mimi
Bali watoto wenu, pia nafsi zenu - Mateso gani haya ee Bwana, unayoteseka Mungu wangu
Lipi baya ee Bwana ulilolitenda - Hatia hiyo wanaiunda, hukumuni wanakuingiza
Nawe hujibu neno, wakubali kufa - Nguvu mwilini zimekutoka, mara ya tatu unaanguka
Teso kubwa ee Bwana, lakusonga sana - Juu msalabani unalia, mateso yamezidi sana
Wasema nina kiu, wanakupa siki