Ee Malkia wa Mbingu Ufurahi
| Ee Malkia wa Mbingu Ufurahi | |
|---|---|
| Performed by | St. Charles Lwanga Yombo Dovya Dsm |
| Album | Kafufuka Mwokozi |
| Category | Pasaka (Easter) |
| Composer | A. J. Msangule |
| Views | 2,937 |
Ee Malkia wa Mbingu Ufurahi Lyrics
Ee malkia wa mbingu Maria ufurahi aleluya
Amefufuka mkombozi amefufuka
Kwani mwanao uliyemchukua ametoka kaburini
Amefufuka mkombozi tufanye shangwe- Mauti ameyashinda Mwokozi amefufuka
Kuzimu ameshatoka Kristu na yuko hai
Shetani ameumbuka na dhambi imefutika - Ni kweli alivyosema ya kwamba angekamatwa
Ateswe mpaka kufa lakini angefufuka
Na sasa amefufuka ushindi tumeupata - Wakristu tuudumishe uhuru tuliopata
Kwa damu aliyomwaga Mwokozi msalabani
Tuache madhambi yetu tudumu katika neema