Ikiwa Twaamini
Ikiwa Twaamini Lyrics
{ Ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa na kufufuka
Vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu
Mungu atawaleta pamoja naye } *2
- Ndugu hatutaki mzijue habari zao waliolala mauti
Msije mkahuzunika kama wengine wasio na matumaini
- Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana
Kwamba sisi tulio hai tutakaosalia
Hata wakati wa kuja kwake Bwana
Hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti
- Kwa sababu Bwana Mwenyezi atashusha kutoka mbinguni
Pamoja na mwaliko na sauti ya malaika mkuu
Na parapanda ya Mungu