Yesu Kashinda Kifo
Yesu Kashinda Kifo Lyrics
- Yesu kashinda kifo, kafufuka leo mfalme wa watu wote
Yesu kashinda kifo, njooni tumwimbie kwa shangwe
Sisi wadhambi alitupenda, katuokoa kaleta na amani
Tuufurahie wema wake njooni wote tukamsifu
- Tufurahi pamoja, Yesu ameshinda nguvu zake shetani
Tufurahie leo, kweli katuokoa sote
Yeye ni Mungu pia Mwokozi, msalabani katuokoa sote
Tuikumbuke huruma yake, tuikumbuke siku zote
- Umeshinda mauti, Yesu umetoka kaburini mzima
Umeshinda mauti, ewe Yesu nakuamini
Ewe Mungu wangu siku zote, unanipenda ingawa nina dhambi
Unijalie neema yako nikufuate siku zote