Mungu Awe Nanyi
| Mungu Awe Nanyi | |
|---|---|
| Performed by | - |
| Category | Harusi |
| Composer | Stanslaus Mujwahuki |
| Views | 5,920 |
Mungu Awe Nanyi Lyrics
{ Mungu awe nanyi, mshirikiane
Mpate amani katika nyumba yenu } *2- Kushirikiana katika furaha,
Katika uchungu ni matakwa ya Mungu. - Na watoto wenu walee vizuri,
Wamjue Mungu ndiye muumba wao. - Na matendo yenu yampendeze Mungu,
Atawajalia uzima wa milele. - Katika uchungu msaidiane,
Mfarijiane ni matakwa ya Mungu. - Mpatapo shida au matatizo,
Mumuombe Mungu atawasaidia.