Pokea Hii Pete
Pokea Hii Pete |
---|
Performed by | - |
Category | Harusi |
Composer | Afred Ossonga |
Views | 5,671 |
Pokea Hii Pete Lyrics
- Pokea hii pete ee mwenzangu,
Iwe ishara ya pendo langu, na uaminifu wangu kwako
{ Nakupenda hakika, nakupenda ajabu
Wewe wangu daima mimi wako wewe
Tutaishi pamoja, tutakula pamoja
Hadi kifo kifike, kitutenganishe } *2
- Jukumu langu ni kukupenda,
Wakati wa raha na wa shida, na wewe kwangu weka heshima
- Safari hii ndefu ya maisha,
Imeanza leo siogope, tutatembea bila kuchoka
- Milima mabonde ya maisha,
Tutapanda tena tutashuka, tukiwa pamoja siku zote