Asante Mama wa Yesu
Asante Mama wa Yesu Lyrics
Asante Mama wa Yesu, asante sana Mama Maria
Uliye muombezi wetu, sisi wanao wa dunia
Baraka za mwana wako, tunazipata kweli Maria
Yote ni kwa ajili yako, muombezi mwema Maria
- Faraja tunazipata, udhaifu unatoweka
Unyonge unatutoka, imani inaongezeka
- Walemavu na wagonjwa, Yesu awafariji sana
Na pia anawaponya, na kuwaongezea neema
- Mapepo wote wabaya, na yule shetani muovu
Haraka wanakimbia, kwa jina la mwanao Yesu
- Uzidi kutuombea, tupate nguvu na uzima
Tusije tukapotea, tufike mbinguni kwa Baba