Asante Mama wa Yesu

Asante Mama wa Yesu
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumAsante Mama wa Yesu
CategoryBikira Maria
ComposerP. F. Mwarabu

Asante Mama wa Yesu Lyrics

Asante Mama wa Yesu, asante sana Mama Maria
Uliye muombezi wetu, sisi wanao wa dunia
Baraka za mwana wako, tunazipata kweli Maria
Yote ni kwa ajili yako, muombezi mwema Maria


1 Faraja tunazipata, udhaifu unatoweka
Unyonge unatutoka, imani inaongezeka

2 Walemavu na wagonjwa, Yesu awafariji sana
Na pia anawaponya, na kuwaongezea neema

3 Mapepo wote wabaya, na yule shetani muovu
Haraka wanakimbia, kwa jina la mwanao Yesu

4 Uzidi kutuombea, tupate nguvu na uzima
Tusije tukapotea, tufike mbinguni kwa Baba

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Zaeni Matunda Mema 5814860
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Sasa Wakati Umefika 7482439
Huniongoza Mwokozi 5814856
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442