Ee Mariamu Wafahamu
Ee Mariamu Wafahamu | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Bikira Maria |
Composer | (traditional) |
Views | 4,831 |
Ee Mariamu Wafahamu Lyrics
- Ee Mariamu wafahamu, wanao wa ugenini
Tupe, Mama, usalama,
Utulinde hapa chini, utulinde hapa chini - Nyota nzuri ya bahari, tuliza dhoruba mbaya,
Na za mwovu, vunja nguvu,
Simwache kutuogofya, simwache kutuogofya - Na memayo jaza nyoyo, za mayatima waombi
Utukaze tuongoze,
Tusichafuke na dhambi, tusichafuke na dhambi - Tukitishwa tukisongwa, na ya mwisho masumbuko
Uje hima na ujima,
Kuopoa watoto wako, kuopoa watoto wako - Ukaako wana wako, Maria Mama Bikira,
Uwinguni kwa amani,
Waonje furaha bora, waonje furaha bora
Recorded by Glorious Singers Tanzania