Malaika Njooni Toka Juu Lyrics

MALAIKA NJOONI TOKA JUU

@ (traditional)

 1. Malaika njooni toka juu, tazameni huyu mtoto
  Imbeni pigeni parapanda, imbeni aleluya

  Aleluya aleluya, aleluya aleluya *2

 2. Kwa sauti nzuri mwimbieni, mtoto Yesu yu horini
  Kwa kinanda na kwa kinubi, imbeni aleluya
 3. Imbeni nyimbo zilizo tamu, kwa mtoto Yesu Bethlehem
  Zipite za ndege wa angani, imbeni aleluya
 4. Watu wote na tutegeane, hoye hoye hoye hoye
  Twendeni tukamsujudie, tuimbe aleluya
Malaika Njooni Toka Juu
COMPOSER(traditional)
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
SOURCETanzania


St. Cecilia
 • Comments