Ni Usiku wa Manane Lyrics

NI USIKU WA MANANE

@ (traditional)

 1. Ni usiku wa manane, mtoto kazaliwa
  Malaika wanaimba, wimbo huu mzuri

  Gloria hosanna in excelsis *2

 2. Wachungaji makondeni na mifugo yao
  Sauti wazisikia toka juu mbinguni
 3. Malaika anashuka toka juu mbinguni
  Kawatoa wasiwasi hao wachungaji
 4. Kwenye mji wa Daudi leo kazaliwa
  Mwokozi wa ulimwengu, ndiye Kristu Bwana
 5. Haya basi twende hima huko Bethlehemu
  Tukaone tukio tuliloambiwa
Ni Usiku wa Manane
COMPOSER(traditional)
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
 • Comments