Pendo la Marafiki
Pendo la Marafiki | |
---|---|
Alt Title | Ninyi Ndinyi Mmenikamilisha |
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Asifiwe Bwana Mungu (Vol 8) |
Category | Love |
Composer | Martin M. Munywoki |
Views | 3,036 |
Pendo la Marafiki Lyrics
- // u t a n g u l i z i //
Ninyi ndinyi mmenikamilisha kamilisha (hadi)
Hadi nikawa hi-vi mi-mi nilivyo (ndugu zangu)
Ni Mungu Baba ndiye aliyetukutanisha (japo)
Japo hatulingani tumekamilishana
{Katika pendo lenu - ndipo nimeelewa jinsi Mungu alivyo
Nimemuona - Mungu macho kwa macho } *2
// k i i t i k i o //[ s ] Nikiwa na njaa -
Ni ninyi marafiki zangu mnimegeao mkate
[ a ] Penye machungu na maumivu makali -
Ni ninyi marafiki zangu mwaniuguza majeraha
[ t ] Nikitawaliwa na hofu -
Ni ninyi marafiki zangu mnaonipa moyo upya
[ b ] Tena nikipotea njia -
Ni ninyi marafiki zangu mwanirudi mwanikosoa
// m a s h a i r i // - Ona tunavyosaidiana hima, wenyewe kwa wenyewe,
Wakati wa furaha hata wa shida
Tumeweka mbali tofauti kidaraja na mali
Bahati iliyoje kuwa pamoja - Ona chuki, wivu, fitina, umimi, havimo kati yetu
Wakati wa furaha hata wa shida
Tumeweka msingi imara usiotikisika
Bahati iliyoje kuwa pamoja
// h i t i m i s h o //
{ Pendo pendo pendo pendo -
pendo letu lidumu milele
Tuombeane tusaidianeni -
waone Mungu kati yetu } *2
Wasitenganishwe - wapendanao
Waombeeni - baraka tele
sitenganishwe - wapendanao
Waombeeni - baraka tele, pendo na lidumu