Twende kwa Yesu
Twende kwa Yesu | |
---|---|
Alt Title | Nakualika Nakualika |
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Asifiwe Bwana Mungu (Vol 8) |
Category | Entrance / Mwanzo |
Composer | John Sway |
Views | 5,864 |
Twende kwa Yesu Lyrics
Nakualika nakualika nawe ndugu yangu
Njoo twende kwake Bwana Yesu (twendeni)
Tukamueleze shida zetu zote (Yeye) anaweza yote
{ Matatizo yetu - tukampe Yeye, tukampe Yeye atatufariji } *2
---MASHAIRI---
- Yeye mwenyewe alisema,
Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao
Na kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha - Yeye mwenyewe alisema,
Ombeni ombeni ombeni mtapewa
Tafuteni mtapata, bisheni hodi mtafunguliwa - Tujikabidhi mbele zake,
Bwana Yesu atatuponya na magonjwa
Magonjwa ya mwili na roho, tukiwa na imani kwake
---HITIMISHO---
- Unangoja nini wewe twende (twende) twende (twende) kwa Yesu
Wala usiogope wala usisitesite,
{ Twende pamoja, usibaki nyuma, twende } *2