Kizazi Hiki

Kizazi Hiki
Alt TitleKizazi cha Nyoka
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumAsifiwe Bwana Mungu (Vol 8)
CategoryTafakari
ComposerT. G. Mwakimata
Views3,239

Kizazi Hiki Lyrics

  1. Nikifananishe kizazi hiki na kitu gani?
    Nashindwa kusema kwa lugha nzuri iliyo fasaha } *2
    { (tazama) kizazi hiki kisicho na upendo,
    kizazi kisicho na huruma,
    chenye moyo wa jiwe (hakika)
    hiki ni kizazi cha nyoka } *2

  2. Kizazi kilichojaa chuki na kisasi,
    ufisadi na moyo wa hila
  3. Kizazi kinachotukuza ushirikina,
    tamaa na anasa za dunia
  4. Ndimi zao zanena upotovu na unafiki,
    na kuliasi JIna la Bwana
  5. Mzabibu uliopanda na kuunyeshea mvua,
    tazama umekuwa mzabibu mwitu
(Harmony by V. Mabula)