Kizazi Hiki Lyrics

KIZAZI HIKI

@ T. G. Mwakimata

Nikifananishe kizazi hiki na kitu gani?
Nashindwa kusema kwa lugha nzuri iliyo fasaha } *2
{ (tazama) kizazi hiki kisicho na upendo,
kizazi kisicho na huruma,
chenye moyo wa jiwe (hakika)
hiki ni kizazi cha nyoka } *2

 1. Kizazi kilichojaa chuki na kisasi,
  ufisadi na moyo wa hila
 2. Kizazi kinachotukuza ushirikina,
  tamaa na anasa za dunia
 3. Ndimi zao zanena upotovu na unafiki,
  na kuliasi JIna la Bwana
 4. Mzabibu uliopanda na kuunyeshea mvua,
  tazama umekuwa mzabibu mwitu
Kizazi Hiki
ALT TITLEKizazi cha Nyoka
COMPOSERT. G. Mwakimata
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMAsifiwe Bwana Mungu (Vol 8)
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYA
TIME SIGNATURE2/4
SOURCEDodoma


(Harmony by V. Mabula)
 • Comments