Yesu ni Mwangaza
Yesu ni Mwangaza | |
---|---|
Alt Title | Mwangaza |
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Asifiwe Bwana Mungu (Vol 8) |
Category | Injili na Miito (Gospel) |
Composer | Bernard Mukasa |
Video | Watch on YouTube |
Views | 5,634 |
Yesu ni Mwangaza Lyrics
- Ndipo ukatema mate, aridhini, ukalifanya tope, mkononi
Ukampaka kipofu , ma-choni, macho yakafunguka, akaona,
Na mimi ni kipofu, nifumbue, macho ya roho yangu, kwa maana{
{ / s/ Mwangaza ni wewe, Mwokozi ni wewe
Mwalimu ni wewe, Kiongozi ni wewe
/ w / Ni wewe mwangaza na ni wewe Mwokozi
Ni wewe mwalimu na ni wewe kiongozi } *2 Yesu
} *2 - Ukamshusha kutoka, kwenye mti, Yule mtu mfupi, wa ushuru
Ukala nyumbani mwake, Zakayo, na ukamfundisha, kugeuka
Naye akakusikia, mwalimu, kageuza mwenendo, kwa maana - Naomba niongoze, ee Yesu, nibadili mwenendo, nigeuke
Njia inipotoshayo, niiache, uniponye usugu, wa moyoni
Dhambi niirudiayo, niishinde, nifundishe niweze, kwa maana