Nitakutukuza Mungu
Nitakutukuza Mungu | |
---|---|
Alt Title | Kwa Kinywa Changu |
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Asifiwe Bwana Mungu (Vol 8) |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | S. E. Mlugu |
Video | Watch on YouTube |
Views | 6,822 |
Nitakutukuza Mungu Lyrics
Kwa kinywa changu Mungu wangu nitakutukuza,
kwa nyimbo nzuri nitaziimba sifa (zako )
Kwa kuwa Mungu wema wako kwangu mimi ni mkuu siwezi kuelezea
{ Sina kitu Bwana cha kukupa (wewe)
kulingana na mema uloyatenda
Naitoa kwako nafsi yangu (Bwana)
nitendee unavyotaka } *2- Kama ni pumzi ya uhai umenipa bure,
Sauti nzuri ya kuimbia, yatoka kwako
Nakurudishia sifa na shukrani - Kama ni elimu, niliyo nayo ni mali yako,
Ujuzi na kazi niliyo nayo vyatoka kwako
Nakurudishia sifa na shukrani - Magonjwa mengi umeniponya ee Mungu wangu,
Na ajali nyingi umenikinga ee Mungu wangu
Nakurudishia sifa na shukrani